Kenya na Sudan Kusini kuimarisha uhusiano

Tom Mathinji, PCS and PCS
1 Min Read

Kenya imejitolea kuimarisha uhusiano kati yake na Sudan Kusini, kwa manufaa ya raia wa mataifa haya mawili.

Rais William Ruto amesema nchi hizo mbili zinaendeleza miradi ya pamoja ya miundo msingi, ili kuimarisha utangamano wa kikanda na kukuza biashara.

Akizungumza katika ikulu ya Nairobi alipofanya mazungumzo na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Rais Ruto alisema Kenya ina nia ya kutekeleza miradi ya miundombinu, chini ya mradi wa Bandari na  Barabara  waLamu-Sudan Kusini na Ethiopia-Transport (LAPSSET), ili kuimarisha uchukuzi, utangamano na ukuzaji wa  biashara ya kikanda kwa ustawi wa pamoja.

Viongozi hao wawili walitia saini Mkataba wa Maelewano kuhusu kuanzishwa kwa kebo ya fibre Optic kando ya barabara ya Eldoret-Juba.

Pia walikubali kukamilisha ujenzi wa barabara ya Nadapal hadi Nakodok yenye umbali wa kilomita 11 na kutumia Mkataba wa Eneo Huria la Biashara barani Afrika ili kuongeza biashara kati ya mataifa hayo mawili.

Aidha, walijadili kuhusu amani na usalama barani Afrika na mzozo wa Sudan, ambapo Rais Kiir aliahidi kuunga mkono juhudi za kukomesha mapigano na kurejesha amani nchini Sudan.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *