Mataifa ya Kenya na Romania yamekubaliana kuendeleza ushirikiano kati yao hadi kwenye sekta za umuhimu kwa nchi zote mbilikama vile kilimo, utunzaji wa mazingira, ushughulikiaji wa majanga na teknolojia ya habari na mawasiliano.
Haya ni kwa mujibu wa Rais William Ruto ambaye pia alisema kwamba biashara na uwekezaji vitaangaziwa zaidi kwa nia ya kusawazisha biashara kati ya nchi hizo mbili.
Mikataba iliyotiwa saini wakati wa ziara ya Rais wa Romania Klaus Werner Iohannis katika ikulu ya Nairobi ni mkataba kuhusu utunzaji wa mazingora na mabadiliko ya tabianchi, mkataba wa ushirikiano kuhusu utunzaji mifugo na usalama wa chakula, mkataba kuhusu utafiti wa kilimo na ushirikiano na mkataba wa taasisi ya kidiplomasia na shule ya huduma za kigeni ya Kenya.
Rais wa Romania Klaus Iohannis aliwasili nchini Kenya jana kwa ziara ya kikazi ya siku 3 anapozuru Afrika kwa mara ya kwanza na baadaye atazuru Tanzania, Cabo Verde na Senegal.
Ziara hiyo ya Afrika ni kati ya Novemba 14 hadi 23, 2023.