Kenya na Italia zafanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya na Italia zimeanzisha mazungumzo yanayolenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya mataifa haya mawili.

Waziri wa biashara Salim Mvurya ametangaza haya leo baada ya kukutana na ujumbe kutoka Italia afisini mwake ukiongozwa na waziri wa biashara wa Italia Roberto Natali.

Mazungumzo hayo yaliangazia zaidi zaidi ushirikiano katika sekta  za kibiashara na ushirikiano hususan, baada ya Kenya kusaini makubaliano ya baina yake na mataifa muungano wa ulaya EU kuhusu uchumi.

Majadiliano hayo yalijikita zaidi kwa swala la kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa kwa wingi na mataifa yote mawili.

Waziri Mvurya amekariri kujitolea kwa serikali ya Kenya kubuni mazingira bora ya kibiahsara kati ya Kenya na Italia, yenye lengo la kubuni nafasi za ajira,kukuza uzalishaji wa humu nchini na kuboresha sekta ya viwanda nchini ili kuongeza tija ya taifa.

Website |  + posts
Share This Article