Kenya na Ethiopia kutatua mizozo ya mpakani

Tom Mathinji, radiotaifa and radiotaifa
1 Min Read

Serikali za Kenya na Ethiopian zimeazimia kufanya kazi kwa pamoja ili kushughulikia kikamilifu mizozo ya mpakani siku za usoni.

Haya yanajiri baada ya taharuki ya wiki mbili kwenye mpaka kati ya nchi hizi mbili kufuatia mauaji ya watu watano na kuibwa kwa mifugo.

Wakati wa mkutano wa amani ulioandaliwa katika sehemu ya Dilloh nchini Ethiopia, eneo la Borana zone ili kuepusha mizozo zaidi ya mpakani, jumbe kutoka nchi hizi mbili zilikariri kujitolea kwao kutafuta amani ya kudumu katika mataifa haya mawili ya upembe wa afrika.

Akiongea kwa niaba ya serikali ya Ethiopia, Mohammed Isaack alisema ipo haja kwa watu wa jamii za Gabra na Borana kuishi kwa utangamano kwa minajili ya kudumisha usalama katika eneo hilo la mpakani.

Takriban mbuzi 900 na punda 44 waliibwa wakati wa uvamizihuo wa tarehe 29 na 30 mwezi Julai huku mbuzi 551 na punda 4 wakipatikana na kukabidhiwa serikali ya Ethiopia.

Website |  + posts
Share This Article