Kenya na China zakubaliana kufanikisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto akutana na Waziri Mkuu wa China Li Qiang.

Rais William Ruto amepongeza China kwa kujitolea kwake kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, hasaa kupitia mradi wa uchukuzi ambao umeboresha miundomsingi nchini Kenya na bara Afrika kwa jumla.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo leo Jumatano alipokutana na Waziri Mkuu wa China Li Qiang Jijini Beijing, Uchina.

Katika mkutano huo, viongozi hao wawili walikubaliana kuharakisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Kenya na China.

“Pia tulikubaliana kuhitimisha makubaliano kuhusu biashara huru kati ya nchi hizi mbili,” alisema Rais Ruto kupitia mtandao wake wa X.

Wakati huo huo, Rais Ruto alitoa wito kwa raia wa Kenya wanaoishi ughaibuni kuunga mkono mipango ya mageuzi inayotekelezwa, hususan katika sekta za Elimu, Kilimo na Afya.

‘Tunaamini kuwa mchango wao utachochea ujumuishaji na ufanisi wa taifa hili.

Rais Ruto aliyasema hayo baada ya kukutana na raia wa Kenya wanaoishi nchini China. Rais Ruto yuko katika ziara rasmi ya kiserikali ya siku nne nchini China.

Website |  + posts
Share This Article