Kenya kuwinda nishani katika fainali tatu Jumamosi

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya itakuwa ikiwinda nishani kwenye fainali tatu katika siku ya kwanza ya makala ya 19 ya mashindano ya riadha duniani mjini Budapest,Hungary siku ya Jumamosi.

Fainali ya kwanza itakuwa matembezi kilomita 20 wanaume kuanzia saa nne kasoro dakika 10 asubuhi .

Bingwa mara tatu wa Afrika Samuel Gathimba Ireri, atajitosa kwenye fainali hiyo akiwa Mkenya pekee akijaribu kuzoa medali baada ya kukosa katika makala ya mwaka uliopita mjini Oregon Marekani.

Saa sita na dakika 5 kutakuwa na mchujo wa mita 400 kwa wanariadha wanne mseto kupokezakana kijiti huku fainaki yake ikianza saa nne na dakika 47 usiku.

Agnes Jebet Ngetich,Irene Kimais na Grace Loibach watatimka fainali ya mita 10,000 kuanzia saa tatu na dakika 47 usiku.

Mashindano mengine kwa Wakenya ni raundi ya kwanza ya mita 1500 kwa wanaume na wanawake na raundi ya kwanza ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji.

Kenya ilizoa medali 10 katika makala ya mwaka jana nchini Marekani kwa dhahabu 2 fedha 5 na shaba 3.

Mashindano yatakayokamilika Agosti 27 yatapeperushwa mbashara na runinga ya taifa KBC Channel 1.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *