Kenya kutuma wanariadha 10 kwa mashindano ya riadha ya ukumbini

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya itatuma kikosi cha wanaroadha 10 kwa makala ya 19 ya mashindano ya riadha ya duniani ya ukumbini yatakayoandaliwa mjini Nanjing, China kati ya tarehe 21 na 23 mwezi huu.

Kikosi cha Kenya kitaongozwa na mshindi wa nishani ya fedha katika mashindano ya ukumbini mwaka 2022 Noah Kibet ,mshindi wa nishani ya fedha ya Afrika Alex Ngeno na Collins Kipruto, watakaotimka

mbio za mita 800, huku Susan Ejore na Vivian Chebet walioshiriki Olimpiki mwaka jana wakijumuishwa katika timu ya wanawake ya mita 800.

Mshindi wa medali ya shaba mwaka jana katika mbio za mita 5,000 Cornelius Kemboi na Purity Kajuju watashiriki mita 3,000.

Kenya ilizoa medali ya shaba pekee katika makala ya mwaka jana mjini Glascow, Scotland, kupitia kwa mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech.

Bingwa wa jumuiya ya madola katika mita 100 Ferdinand Omanyala hatashiriki mashindano ya mwaka huu ili kujiandaa kwa mashindano ya dunia ya Tokyo Septemba mwaka huu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *