Serikali ya Kenya imetangaza kuondoa sharti la leseni ya kufanya kazi humu nchini kwa raia wa kigeni wanaotokea katika mataifa wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki-EAC.
Waziri wa mawaziri ambaye pia ni waziri wa mashauri ya kigeni Musalia Mudavadi, amefichua kuanzia mwaka ujao raia wanaotokea mataifa ya Uganda,Tanzania,Rwanda,Burundi,DR Congo,Somalia na Sudan Kusini hawatahitaji stakabadhi hiyo ili kuishi na kufanya kazi humu nchini.
Kenya ni nchi ya pili katika jumuiya ya EAC kuondoa hitaji la leseni ya kufanya kazi kwa wanachama wake,baada ya Rwanda.