Kenya itashuka uwanjani Mamboleo, kaunti ya Kisumu Jumanne asubuhi kwa mchuano wa pili wa kundi A dhidi ya Rwanda, kuwania kombe la CECAFA kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18.
Ushindi kwa Kenya utawafuzisha kwa hatua ya nusu fainali, baada ya kushinda mechi ya kwanza mabao 5 kwa nunge dhidi ya Sudan.
Rwanda pia walipata ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya Somalia.
Mechi ya pili ya siku itang’oa nanga saa nane adhuhuri kati ya Somalia na Sudan.
Mashindano hayo yanayoshirikisha timu nane yanarejea Jumanne baada ya mapumziko siku ya Jumatatu.