Kenya kukabiliana na Burundi kusaka tiketi ya AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 itashuka dimbani  Azam Sports Complex  jijini Dares Salaam Tanzania leo jioni  kwa nusu fainali ya pili ya  michuano ya CECAFA.

Nusu fainali hiyo itakuwa ya pili baada ya Burundi na wenyeji Tanzania, watakaokabana koo kuanzia saa tisa alasiri uwanjani KMC.

Kenya almaarufu Rising Stars, ilifuzu kwa nufu fainali baada ya kuongoza kundi A kwa pointi 10,ikifuatwa na Tanzania kwa alama 9.

Upande wa pili wa sarafu Uganda waliongoza kundi B kwa alama 7 ,moja zaidi ya Burundi iliyomaliza ya pili.

Timu mbili zitakazofuzu kwa  fainali zitajikatia tiketi kwa mashindano ya kuwania kombe la Bara Afrika (AFCON) mwaka ujao.

Website |  + posts
Share This Article