Kenya itawalinda wawekezaji, asema Rais Ruto

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali inabuni mazingira bora yatakayovutia uwekezaji wa kigeni humu nchini

Rais William Ruto amesema serikali yake pia itaboresha sera zake ili kuzifanya ziwezeshe utendakazi wa makampuni nchini.

“Tutaendelea kuwasiliana na wawekezaji ili kufanya sheria zetu kuwa zinazounga mkono biashara. Hii itachochea ukuaji wa biashara hizo.”

Rais Ruto aliyasema hayo leo Alhamisi katika Ikulu ya Nairobi, wakati wa mkutano wa ujumbe wa biashara kati ya Kenya na Saudi Arabia.

Ukiongozwa na Waziri wa Uwekezaji wa Saudi Arabia Khalid Al Falih, ujumbe huo — uliojumuisha zaidi ya kampuni kubwa 30 — ni moja ya makundi makubwa ya kibiashaa kuwahi kuitembelea Kenya.

Rais Ruto alisema Kenya ipo mahali pazuri kimkakati na kufanya iwe rahisi kwa makampuni kupata masoko mazuri katika kanda hii na barani Afrika kwa jumla.

Mawaziri Moses Kuria wa Biashara na Uwekezaji, Davis Chirchir wa Nishati na Florence Bore wa Leba walikuwepo wakati wa mkutano huo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *