Kenya ingali na imani ya kukabidhiwa maandalizi ya mashindano ya Riadha Duniani 2029

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya ingali na matumaini ya kushinda maandalizi ya mashindano ya Riadha Duniani ya mwaka 2029 au mwaka 2031.

Mwandalizi wa makala hayo mawili atatangazwa Septemba 15 mjini Budapest,Hungary.

Kenya inawania maandalizi ya mashindano hayo pamoja na Rome,Italia,Munich,Ujerumani na London,Uingereza.

Mashindano hayo hayajawahi andaliwa barani Afrika tangu yaanzishwe.

Ni mara ya pili kwa Kenya kujaribu bahati ya kuandaa mashindano hayo bada ya kupoteza maandalizi ya mwaka 2025 kwa  Tokyo,Japan.

Mashindano ya Riadha Duniani mwaka ujao yataandaliwa  Beijing,Uchina.

Share This Article