Kenya huenda ikakumbwa na uhaba wa mafuta

Licha ya serikali kukiri kuwepo kwa mafuta ya kutosha nchini, imebainika kuwa huenda Kenya ikakumbwa na uhaba wa bidhaa hiyo kuanzia mwisho wa mwezi Machi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya huenda hivi karibuni ikakumbwa na uhaba mkubwa wa mafuta kutokana na mashambulizi yanayoendelea  nchini Iran. 

Mashambulizi hayo yanaendeshwa kwa pamoja na majeshi ya Israel na Marekani.

Hii inatokana na hatua ya majeshi ya Marekani na Israel kushambulia kituo kikubwa cha Adnoc, kilicho mjini Abu Dhabi na kinachozalisha mafuta mengi yanayotumika na Kenya na Uganda.

Licha ya serikali kukiri kuwepo kwa mafuta ya kutosha nchini, imebainika kuwa huenda Kenya ikakumbwa na uhaba wa bidhaa hiyo kuanzia mwisho wa mwezi Machi.

Wizara ya Nishati kwenye taarifa yake ya awali ilikuwa imekiri kuwa Kenya ina akiba ya kutosha ya mafuta yatakayotumika hadi mwishoni mwa mwezi ujao.

Share This Article