Kenya, Africa CDC kushirikiana kuboresha mfumo wa afya

Martin Mwanje
1 Min Read

Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa barani Afrika, Africa CDC ni rasilimali muhimu na mshirika kwa afya ya umma humu nchini na kote barani humo.

Rais William Ruto anasema Kenya inatazamia kuboresha taasisi zake za afya kupitia ushirikiano na kituo hicho katika nyanja kama vile mifumo ya maabara, kujiandaa kwa hali za dharura na ushughulikiaji wa hali kama hizo, utafiti na uangalizi.

Rais Ruto aliyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC Dkt. Jean Kaseya katika Ikulu ya Nairobi.

Wakati wa mkutano huo, viongozi hao walijadili uongezaji wa uwezo wa mfumo wa afya wa nchi hii.

Walikubaliana kuwezesha kuanzishwa kwa afisi za kikanda za kituo hicho jijini Nairobi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *