Mamlaka ya kitaifa ya barabara kuu nchini KeNHA, imetangaza usumbufu wa muda wa trafiki katika mzunguko wa Haile Selassie kwenye barabara ya Uhuru Highway.
Usumbufu huo unatarajiwa kati ya Novemba 28, 2024 na Januari 17, 2025, wakati mapito ya chini kwa chini ya wanaotembea kwa miguu yatakuwa yanajengwa.
Waendeshaji magari wameshauriwa kufuata mpango wa kusimamia trafiki, alama za barabarani na kushirikiana na maafisa wa polisi na trafiki watakaokuwepo.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya mamlaka ya KeNHA kutangaza usumbufu wa trafiki katika makutano ya barabara ya Gitaru kwenye barabara ya Waiyaki.
Hatua hiyo ililenga kutoa fursa kwa ujenzi wa sehemu ya barabara hiyo kati ya Novemba 19 na Disemba 19, 2024.