Halmashauri ya usimamizi wa barabara kuu hapa nchini KeNHA, imeanza ukarabati wa daraja la Mbogolo katika barabara kuu ya Mombasa – Kilifi, lililosombwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa inayoshuhudiwa hapa nchini.
Kupitia kwa taarifa katika mtandao wa X, KeNHA ilisema viwango vya maji vimepungua katika eneo hilo, na kwamba hali ya kawaida ya uchukuzi itarejea katika muda wa saa 24 zijazo.
“KeNHA inafahamisha ummakuwa viwango vya maji katika daraja la Mbogolo vimepungua. KeNHA imeanza ukarabati katika eneo hil. Halmashauri hii inatarajia kufungua sehemu hiyo katika muda wa saa 24 zijazo,” halmashauri hiyo ilisema kupitia mtandao wa X siku ya Jumamosi.
Barabara ya Mombasa-Kilifi ilifungwa Jumamosi asubuhi baada ya daraja hilo kusombwa na maji ya mafuriko, na kusanbaratisha shughuli za uchukuzi kati ya Mombasa na Kilifi.