Kendrick Lamar kutumbuiza kwenye Super Bowl

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki Kendrick Lamar Duckworth maarufu kama Kendrick Lamar ndiye atatumbuiza wakati wa mapumziko kwenye awamu ya 59 ya shindano la kila mwaka la soka nchini Marekani Super Bowl.

Lamar alitangaza hayo Jumapili Septemba 8, 2024 kupitia mitandao ya kijamii.

Tamasha hilo fupi katikati ya mchezo wa soka huchukuliwa kuwa muhimu sana na wasanii wa Marekani na wadadisi wanahisi Lamar anatosha kwani amewahi kushinda tuzo 17 za Grammy na nyimbo kadhaa zilizofanya vizuri.

Kwenye video ya tangazo lake, Lamar alionekana akiwa amesimama kwenye uwanja wa michezo na mbele ya bendera ya Marekani. Alihimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi wakati huo akisema fursa ya kushinda ni moja tu.

Awamu hiyo ya 59 ya Super Bowl itaandaliwa Februari 9 2024 na waandalizi zamu hii wameamua kutangaza mtumbuizaji mapema tofauti na ilivyokuwa awali.

Mwaka jana mwanamuziki Usher ndiye alitumbuiza kwenye awamu ya 58 ya Super Bowl, huku Rihanna akitumbuiza kwenye awamu iliyotangulia ya 57.

Mtumbuizaji mkuu huwa na fursa ya kualika wanamuziki wengine na mashabiki wanasubiri kuona Lamar mwenye marafiki wengi katika tasnia ya muziki atachagua nani.

Share This Article