Kenya Commercial Bank wangali kushikilia kukutu msimamo wa ligi kuu ya Kenya licha ya kuambulia kichapo cha mabao mawili kwa nunge jana na Shabana FC .
Ushindi wa jana umewakweza Shabana hadi nafasi ya tano ligini kwa pointi 20,alama 4 nyuma ya vinara.
Tusker FC ni ya pili kwa pointi sawa 24 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bidco United,wakati Bandari FC ikikalia nafasi ya tatu kwa alama 22 baada ya kwenda sare ya 2-2 dhidi ya Mathare United jana.
Police FC iliyowakung’uta mabingwa watetezi Gor Mahia bao moja bila jibu ni ya nne kwa alama 20 sawa na Shabana walio katika nafasi ya tano.
AFC Leopards ni ya sita ligini kwa alama 19 sawia na Mara Sugar walio nafasi ya saba nao Gor Mahia,Sofapaka na Kariobangi Sharks wanashikilia nafasi za 8,9 na 10 mtawalia.