KCB na Prisons kushikana mashati mashindano ya Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Ligi ya Kenya KCB, na watani wa jadi Prisons watachuana na wenzao Kenya Prisons katika mechi ya kuwania nafasi ya tano na sita kesho, kwenye mashindano ya kilabu bingwa Afrika, yanayoendelea mjini Abuja, Nigeria.

KCB wameishinda APR ya Rwanda leo seti 3-2 za 27-25, 25-20, 21-25, 20-25 na 15-9 katika mchuano kuwania nafasi ya 5 hadi nane .

Upande wao magereza wameibwaga LTV kutoka Cameroon seti 3-0 leo za 25-18, 25-14 na 25-16 katika mechi nyingine ya kuwania nafasi za 5 hadi 8.

Timu hizo za Kenya zilishindwa katika nusu fainali na wapinzani wa kutoka Misri.

Website |  + posts
Share This Article