KBC na NCIC kushirikiana kueneza amani nchini

Martin Mwanje
1 Min Read
Maafisa wa KBC na NCIC walipokutana na kukubaliana kushirikiana kueneza ujumbe wa amani nchini

Shirika la Utangazaji nchini, KBC litashirikiana na Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Maridhiano, NCIC, kueneza amani humu nchini. 

Chini ya ushirikiano huo, taasisi hizo mbili zitaeneza amani katika ngazi za kitaifa, kaunti na vijijini.

Maafikiano hayo yamefikiwa wakati timu ya NCIC ilipomtembelea Mkurugenzi Mkuu wa KBC Agnes Kalekye afisini mwake leo Ijumaa.

Timu hiyo iliongozwa na kaimu Afisa Mtendaji wa NCIC, Harrison Kariuki.

 

Wengine waliokuwapo wakati wa mkutano huo ni Mhariri Mkuu wa KBC  Samuel Maina, Afisa Mkuu wa Mawasiliano wa NCIC, Rosemary Were na Afisa Mkuu wa Sheria wa tume hiyo Mwikamba Gitonga.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *