Serikali ya kaunti ya Turkana kwa ushirikiano na Millennium Water Alliance na mpango wa DRIP FUNDI, zimeanzisha mpango wa kuhakikisha upatikanaji wa maji safi katika kaunti hiyo.
Uwekaji mfumo wa kusafisha maji kutumia dawa aina ya chlorine katika mfereji wa kisima cha Nakoyo, wadi ya Kakuma, unaashiria hatua kubwa ya kuhakiksha jamii ya eneo hilo inapata maji safi.
Afisa wa maji katika kaunti ndogo ya Turkana Magharibi, alitangaza umuhimu wa mpango huo katika kukabiliana na magonjwa yatokanayo na maji.
“Mfumo huo wa kuweka dawa ya chlorine, unatoa fursa ya upatikanaji wa maji safi na unaimarisha viwango vya ubora vya maji,” alisma afisa huyo.
Mradi wa DRIP FUNDI, amao pia unalenga kuimarisha upatikanaji wa maji, unapiga jeki mfumo wa kuweka dawa aina ya chlorine katika mifereji ya maji ya visima katika visima saba kwenye kaunti hiyo.