Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken atazuru Israel leo Alhamisi kama njia ya kuunga mkono nchi hiyo inapokabiliana na wanamgambo wa Hamas kutoka Palestina katika ukanda wa Gaza.
Binken pia anatarajiwa kukutana na kiongozi wa Palestina katika harakati za kutafuta suluhu kwa mzozo huo.
Wakazi wa ukanda wa Gaza wanakumbwa na ukosefu mkubwa wa chakula, maji na mafuta huku makabiliano baina ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Hamas katika ukanda wa Gaza yakiingia siku ya sita.
Watu zaidi ya 2,500 wameangamia na wengine zaidi ya 10,000 kujeruhiwa kwenye makabiliano hayo.
Watu wengine laki nne wameripotiwa kupoteza makazi.