Katibu Mkuu wa chama cha UDA Hassan Omar, anatarajiwa kufika mbele ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kutokana na matamshi tata aliyotoa kuhusu wapiga kura waliofariki.
Tume hiyo, inataka ufafanuzi kuhusu matanshi hayo yaliyotolewa wakati wa mkutano wa awali wa kisiasa katika eneo la Jomvu kaunti ya Mombasa mwezi uliopita.
Kulingana na IEBC, swala hilo litashughulikiwa chini ya kanuni za kimaadili kwenye sheria ya uchaguzi ya mwaka 2011.
Huku taifa hili likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, IEBC imetoa wito kwa viongozi wa kisiasa, wananiaji wa nyadhifa za kisiasa , wafuasi na wadau wote kuwajibikia matamshi na mienendo yao.
Wakati huo huo, tume hiyo iliwahimiza kubuni mazingira bora ya uchaguzi yaliyojikita kwenye amani, kuvumiliana, uzingatiaji wa mfumo wa sheria na ushiriki wa kidemokrasia.