Mafisa wa polisi wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati aina ya Cocaine katika kituo cha mpakani cha Malaba.
Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), mihadarati hiyo ni ya thamani ya shilingi milioni 2.19.
Mihadarati hiyo ilinaswa wakati basi la kampuni ya Simba Coach lenya nambari za usajili KDG 093H, lililokuwa likielekea Nairobi kutoka Kampala, liliposimamishwa kwa ukaguzi wa kawaida.
Wakati wa ukaguzi huo, maafisa walipata mzigo ambao haukuwa na mwenyewe, walipokuwa wakilikagua, dereva na kondakta wa basi hilo walitoroka.
Maafisa wa kukabilana na ulanguzi wa mihadarati katika kituo cha Malaba, walichukua mzigo huo na baada ya kulichunguza walipata tembe nane za mihadarati inayoshukiwa kuwa cocaine, zenye uzani wa gramu 547.99 grams, gharama yake ikikadiriwa kuwa shilingi milioni 2,191,960.
Hata hivyo utingo wa basi hilo Meshack Medalack, alikamatwa kuhusiana kisa hicho, huku maafisa hao wakimtafuta dereva wa basi hilo aliyetambuliwa kuwa John Musimbi.
Basi hilo linazuiliwa katika kituo cha mpakani cha Malaba, usimamizi wa basi hilo ukiwatafutia wasafiri basi lingine.