Edward Ngeywa Katama, amesema anaelewa changamoto inayoambatana na Uenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, ila yuko tayari kukabiliana nazo.
Katama alisema haya Jumatatu jioni alipokuwa wa mwisho miongoni mwa watu wanne waliosailiwa na jopo la uetuzi ulioanza leo eneo la South C.
Ngeywa amesema hatari za kazi hiyo ni nyingi, lakini anapendekeza kuimarishwa kwa teknolojia na mikakati ya kupanga uchaguzi na kuharakisha zoezi la kuhesabu na kutangaza matokeo ya kura za uchaguzi mkuu.
Usaili huo utaingia siku ya pili kesho, ambapo Erastus Edung atakuwa wa kwanza kuhojiwa kuanzia saa mbili unusu, akifuatwa na Francis Kissinger kuanzia saa tano, naye Jacob Ngwele aingie kuanzia saa nane adhuhuri, kisha Joy Masinde afunge siku kuanzia saa kumu unusu.
Shughuli za usaili itakamilika Jumatano.