Mbunge wa Kasarani Ronald Karauri ametangaza azma ya kuwania Ugavana wa kaunti ya Nairobi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Karauri amesema nia yake endapo atachaguliwa ni kubadulisha hali ya jiji la Nairobi huku akitarajia kupata uungwaji mkono kutoka kwa wapiga kura wa eneo lake la Kasarani.
Kiti cha Ugavana wa Nairobi kinamezewa mate na wanasiasa kadhaa akiwemo aliyekuwa waziri wa zamani wa biashara Moses Kuria, Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na Mwanahabari Tony Gachoka.
Aidha, Gavana wa sasa Jonhson Sakaja analenga kutetea kiti chake kwa muhula mwingine.