Kamusinga, Butere na Kesogon washinda FEASSSA

Dismas Otuke
1 Min Read

Wavulana na wasichana wa shule za Kamusinga na Butere mtawalia, wamenyakuwa ubingwa wa michezo ya vikapu kwa mashindano ya Afrika Mashariki baina ya shule za upili mjini Mbale nchini Uganda.

Kamusinga iliilaza Seroma (UG) vikapu 14 kwa 13 nayo Butere ikaipiku St.Noa (UG) vikapu 17 kwa 15.

Kesogon nayo iliwazidi nguvu mabingwa wa humu nchini – Kwanzanze katika mchezo wa Voliboli seti tatu kwa nunge za 25:16, 25:18 na 25:17.

Kwenye magongo ya akina dada, St.Joseph walishinda tuzo hilo baada ya mechi zote za mzunguko.

Katika soka, Musingu walizawadiwa medali ya shaba kufuatia ushindi wa magoli matatu kwa mawili dhidi ya Bukedea( UG).

Amus College ndio mabingwa wapya wa taji la mwaka huu walipowalaza mabingwa watetezi St.Mary’s Kitende goli moja.

Vile vile, Laiser Hill walishindwa na Amus katika mchezo wa vikapu vya wachezaji watano kila upande alama 54 Kwa 51.

Mashindano hayo, yamekamilika rasmi hii leo. Mwaka ujao yataadaliwa nchini Kenya mjini Kakamega.

Share This Article