Kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya LG nchini Kenya imetangaza kurejea kwa ofa za Black Friday itakayoendelea hadi mwishoni mwa mwezi Novemba.
Kwenye kampeini hiyo, wateja wanaonunua vifaa vya LG watapata punguzo la bei kati ya shilingi 3,000 na 25,000 kwa vifaa umeme kadhaa ikiwemo runinga, jokofu, mashine za kufua nguo, viyoyozi na vifaa vya muziki.
Kulingana na Meneja Mkurugenzi wa LG ukanda wa Afrika Mashariki Dongwong Lee, ofa hiyo ni njia moja ya kuwashukuru wateja wanaonunua bidhaa za LG kote nchini.