Kampuni ya uchukuzi wa ndege nchini Uganda, Uganda Airlines, ilifutilia mbali safari za kuelekea jijini Kinshasa nchini DRC kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo.
Kulingana na kampuni hiyo, sababu kuu ya kufutilia mbali safari hizo ni usalama na ikahakikishia wateja waliokuwa wamelipia safari hizo kwamba inafuatilia matukio nchini Congo.
Hali ya taharuki imeshuhudiwa nchini DR Congo huku ripoti za kuongezeka kwa machafuko zikisababisha kukatizwa kwa usafiri na hata uendeshaji wa biashara.
Uganda Airlines haikufafanua wakati safari za kuelekea Kinshasa zitarejelewa lakini inasisitiza kuhusu umuhimu wa usalama wa abiria.
Wasafiri walioathiriwa na hatua hiyo walishauriwa kuwasiliana na kampuni kwa usaidizi wowote ambao huenda wakahitaji.
Wameshauriwa pia kufuatilia majukwaa ya Uganda Airline ya mawasiliano zikiwemo akaunti za mitandao ya kijamii na hata tovuti ili kupata habari.
 
					 
				 
			
 
                                
                              
		 
		 
		 
		