Kampuni ya Skyward yazindua safari za kutoka Nairobi hadi Migori

Marion Bosire
1 Min Read
Mama Ida Odinga, Akothee na Waziri Murkomen

Kampuni ya usafiri wa ndege kwa jina Skyward imezindua safari za ndege kati ya uwanja wa ndege wa Wilson jijini Nairobi na uwanja mdogo wa ndege wa Lichoti huko Migori.

Uzinduzi wa safari hizo uliongozwa na waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen na mama Ida Odinga mke wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Wawili hao na viongozi wengine waliabiri ndege hiyo ya Skyward kuelekea Migori ambapo waziri Murkomen anatarajiwa kuzindua rasmi uwanja mdogo wa ndege wa Lichoti.

Awali Gavana wa kaunti ya Migori Ochillo Ayako aliongoza ukaguzi wa uwanja huo mdogo wa ndege kabla ya uzinduzi wake leo.

Gavana Ayako akiongoza ukaguzi wa uwanja wa Lichota

 

Mwanamuziki Akothee ambaye ni balozi wa kampuni hiyo ya Skyward Express ni mmoja wa wahudumu wa ndege kwenye safari hiyo ya kwanza kuelekea Migori.

Kampuni ya Skyward awali ilitoa taarifa kwamba safari za kuelekea na kutoka Migori zitakuwa tatu kila wiki siku ya Jumatatu, Jumatano na Ijumaa na abiria watakuwa wanalipa shilingi 7,600.

Skyward Express hufanya pia safari nyingine za ndege kwa aboria kutoka uwanja wa ndege wa Wilson hadi Kitale,Kakamega, Eldoret, Lodwar, Mombasa, Lamu, Malindi na Ukunda.

Website |  + posts
Share This Article