Kalonzo asema wataendelea kukosoa serikali

Marion Bosire
1 Min Read

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amesema kwamba kama viongozi wa upinzani, wataendelea kukosoa serikali ya Kenya Kwanza.

Hata hivyo alifafanua kwamba hawatatumia vurugu kufanya hivyo bali watafanya hivy kwa njia ya amani.

“Tutaendelea kukosoa serikali ya Kenya Kwanza. Lakini hatutachukua panga au jiwe tupigane na wakenya wenzetu. Tutafanya hivyo kwa njia ya amani.” alisema Musyoka.

Aliendelea kusema kwamba wakati wa mazungumzo magumu unakuja na wakenya ni lazima wawe huru kutagusana na miungano waipendayo ya kisiasa.

“Tuna wafanyabiashara ambao wanaogopa kuonekana na wanasiasa wa upinzani kwa sababu maafisa wa kukusanya ushuru watatumwa kwao kuwahangaisha.” alidai kiongozi huyo wa Wiper.

Kalonzo alisema pia kwamba hawataondokea changamoto ya kukomboa Kenya na kwamba watasimama na wakenya kurejesha nchi hii.

Taarifa hiyo ya kiongozi wa Wiper ilipachikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Alizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo ya kwanza kabisa ya kila mwaka ya balozi wa amani kitaifa kutoka kwa baraza la mashirika ya kijamii na bodi ya ushauri ya wapatanishi.

Hanifa Safia Adan naye alipokea tuzo ya amani  kutokana na juhudi zake za uanaharakati wa kizazi kipya.
Hafla hiyo iliandaliwa katika afisi za Kalonzo Musyoka.
Share This Article