Kakamega yaandaa kongamano la uwekezaji

Marion Bosire
1 Min Read

Kaunti ya Kakamega inaandaa kongamano la kimataifa la uwekezaji lililoanza leo Jumanne katika Chuo Kikuu cha Masinde Muliro.

Kongamano hilo la siku nne litamalizika Ijumaa wiki hii na limewaleta pamoja washiriki 2000.

Litafunguliwa na Rais William Ruto na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Balozi wa Marekani humu nchini Meg Whitman.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Uwekezaji na Maendeleo Elizabeth Asichi, kaunti ya Kakamega itatumia fursa hiyo kupata wawekezaji watakaopiga jeki miradi mbalimbali kama vile ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Kakamega iliyo na vitanda 750.

Aliishukuru serikali ya kitaifa kwa msaada wa kumaliza uga wa Bukhungu utakaotumiwa kuandaa mashindano ya CHAN mwakani na utavutia wawekezaji na biashara nyingine.

Asichi amewataka wakazi wa Kakamega kutumia kongamano hilo kujiimarisha kimawazo na kibiashara.

Kongamano hili linajiri baada ya kongamano sawia kuandaliwa katika kaunti ya Homa Bay siku chache zilizopita.

Share This Article