Kagame arai ushirikiano wa Mawaziri wake

Dismas Otuke
0 Min Read

Rais wa Rwanda Paul Kagame amewataka Mawaziri wake kushirikiana katika utendakazi wao. 

Amesema hatua hiyo itaisadia serikali yake kuafikia malengo yake ya  miaka mitano.

Kagame alisema hayo mapema wiki hii aliposhuhudia kuapishwa kwa Mawaziri 21 pamoja na maafisa wengine 9 wa serikali.

Rais huyo alikula kiapo cha kuiongoza Rwanda kwa muhula mpya wa miaka mitano, baada ya kukamilisha mihula miwili ya miaka saba kila mmoja afisini.

Share This Article