Justin Baldoni aishtaki New York Times akidai fidia

Baldoni na Lively waliigiza pamoja kwenye filamu "It Ends with Us", ambapo Baldoni pia alihudumu kama mwelekezi.

Marion Bosire
2 Min Read
Justin Baldoni, Mwigizaji

Mwigizaji wa Marekani Justin Baldoni ameishtaki gazeti la New York Times akidai fidia ya dola milioni 250, baada ya gazeti hilo kuashiria kwamba yeye na wengine walianzisha mchakato wa kumharibia sifa mwigizaji Blake Lively.

Baldoni na Lively waliigiza pamoja kwenye filamu “It Ends with Us”, ambapo Baldoni pia alihudumu kama mwelekezi.

Lively alikuwa amemshtaki Baldoni kuhusiana na kile alichokitaja kuwa unyanyasaji wa kingono, kesi iliyoangaziwa mno na New York Times kwenye chapish analolalamikia Baldoni.

Baldoni analaumu gazeti hilo kwa kumharibia sifa, mwingilio wa faragha, ahadi za uongo na ukiukaji wa mkataba wa uelewa akisema gazeti hilo lilichagua mambo fulani kwenye kesi hiyo na kuacha mengine na hivyo kupotosha wasomaji.

Yeye ni mmoja wa watu 10 ambao wanashtaki gazeti hilo kutokana na chapisho hilo wakiwemo Melissa Nathan na Jennifer Abel, ambao walitajwa humo.

Baldoni na wenzake wanasema kwamba Lively anatumia tuhuma za unyanyasaji kujaribu kudhibiti filamu yao ya ‘It Ends with Us’.

Mwigizaji huyo na mwelekezi amemshtaki pia mume wa Lively aitwaye Ryan Reynolds, akisema alimzomea kwa kile alichokitaja kuwa udhalilishaji wa mkewe kutokana na unene wake.

Wakili wa Baldoni kwa jina Bryan Freedman naye anashikilia kwamba Blake ndiye anamharibia sifa mteja wake na wenzake huku msemaji wa New York Times akisema kwamba chapisho lao liliafiki viwango hitajika.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *