Juliet Zawedde kumpeleka Jose Chameleone ng’ambo kwa matibabu

Zawedde, alisema hayo jana alipomtembelea Jose Chameleone katika hospitali ya Nakasoro jijini Kampala ambapo amelazwa.

Marion Bosire
1 Min Read

Mfanyabiashara wa asili ya Uganda anayeishi Boston, Massachusetts nchini marekani Juliet Zawedde, atafadhili usafiri na matibabu ya mwanamuziki Jose Chameleone ng’ambo.

Haya ni kulingana na mtangazaji Isaac Daniel Katende maarufu kama Kasuku, ambaye anasema alifahamu hayo kupitia taarifa kutoka hospitalini alikolazwa Jose Chameleone.

Kulingana na Kasuku Chameleone atatibiwa nchini Marekani.

Jumatatu Disemba 16, 2024, Zawedde alimzuru Chameleone, hospitalini Nakasero, katika jiji kuu la Kampala.

Bad Black, alikuwa amedai awali kwamba Chameleone anajisingizia kuwa mgonjwa ili kukwepa kulipa deni kubwa alilonalo.

Ritah Kaggwa ambaye ni mwanamitandao maarufu nchini Uganda baadaye alifafanua kwamba alikuwa amezungumza na Zawedde, aliyemwelezea kwamba yuko Uganda kwa likizo.

Juliet Zawedde alijitenga pia na madai kwamba ana deni kubwa la Jose Chameleone, akisema pesa anazotumia na atakazotumia kumpeleka kwa matibabu ni zake na kwamba Chameleone hana deni lake.

Alisema Jose ni mgonjwa kikweli, anapambania maisha yake na anachohitaji ni usaidizi wa kimatibabu na kimawazo na wala sio minong’ono mitandaoni.

Juliet Zawedde na Jose Chameleone wamekuwa marafiki kwa muda mrefu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *