Judith Suminwa Waziri Mkuu mwanamke wa kwanza DRC aapishwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Judith Suminwa Tuluka ambaye ni Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, aliapishwa jana katika bunge la kitaifa .

Bi Tuluka aliapishwa pamoja na maafisa wengine 54 wa serikali iliyotangazwa Mei 29.

Serikali hiyo mpya inayoongozwa na Rais Felix Tshisekedi inawajumuisha Waziri Mkuu,manaibu sita wa Waziri Mkuu na Mawaziri 10.

Waziri Mkuu mpya kwenye hotuba yake baada ya kula kiapo alisema anajivunia kuwa mwanamke wa kwanza kuweka historia kushikilia wadhfa huo, akiahidi kubuni nafasi za ajira milioni 2.6.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *