John Okulo ateuliwa meneja mkurugenzi mpya wa benki ya Sidian

Dismas Otuke
1 Min Read

Benki ya Sidian imemteua John Okulo kuwa Meneja Mkurugenzi mpya kuanzia Mei mosi mwaka huu.

Okulo anajiunga na Sidian kutoka KCB alipohudumu katika wadhifa wa mkurugenzi wa mashirika kwa zaidi ya miaka 28.

Okulo anamrithi Chege Thumbi, atakayestaafu Juni 30, baada ya kuwa usukani kwa miaka tisa.

Sidian Bank chini ya uongozi wa Thumbi ilipandishwa ngazi hadi kiwango cha pili cha taasisi za kifedha na kufungua matawi zaidi ya 50 nchini.

 

Share This Article