JLo ahusishwa kwenye filamu mpya – Office Romance

alionekana katika eneo moja la makazi ya kifahari huko New Jersey Ijumaa akiwa na wenzake katika harakati za maandalizi ya Office Romance.

Marion Bosire
2 Min Read
James Olmos na Jennifer Lopez

Mwanamuziki na mwigizaji Jennifer Lopez maarufu kama JLo ni mmoja wa wahusika wakuu wa filamu inayoendelea kuandaliwa kwa jina “Office Romance”.

Lopez alizungumzia filamu hiyo kweye Instagram ambapo alimkaribisha mwigizaji James Olmos kwa uigizaji wa kazi hiyo.

Wawili hao wanakutana tena baada ya kuigiza pamoja kwenye filamu ya mwaka 1997 kuhusu mwimbaji Selena Quintanilla-Pérez.

Lopez aliigiza kama Selena huku Olmos akiigiza kama babake Selena kwa jina Abraham Quintanilla.

Olmos anaigiza tena kama babake Lopez kwenye hii filamu mpya.

Brett Goldstein anahusika pia katika filamu hiyo ambayo ameiandika kwa ushirikiano na Joe Kelly huku Ol Parker akiwa mwelekezi wao.

Jlo alionekana katika eneo moja la makazi ya kifahari huko New Jersey Ijumaa akiwa na wenzake katika harakati za maandalizi ya Office Romance.

Alikuwa akitembea kutoka kwenye mkahawa mmoja uliokuwa umekodishwa kwa ajili ya maandalizi ya filamu hiyo akielekea kwenye gari lake huku akiwa ameinamisha kichwa.

Mrembo huyo amerejelea kazi baada ya talaka yake na Ben Affleck, wiki chache baada ya Affleck kuizungumzia kwenye mahojiano na jarida la GQ.

Alirejelea uhusiano wao kama wa watu wawili ambao walikuwa wakijaribu kutafuta maisha na ambao huenda walihitaji ushauri nasaha kuhusu ndoa.

katika mahojiano hayo, Ben alikiri kwamba alijihisi mwenye aibu na aliye katika hatari kutokana na talaka hiyo ndio maana hakuizungumzia kwa muda mrefu.

Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi mwaka 2002 hadi 2004 baada ya kukutana kwenye maandalizi ya filamu iitwayo ‘Gigli’.

Mwaka 2021 walirudiana, wakafunga ndoa mwaka 2022, wakatengana 2024 kabla ya kukamilisha talaka yao Januari 2025.

Website |  + posts
Share This Article