Kwa mara ya pili wachezaji wa klabu ay USM Alger ya Algeria walidinda kuingia uwanjani kwa marudio ya nusu fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya RS Barkane ya Morocco.
Mzozo huo ulianza moja iliyopita wakati wachezaji wa Barkane walipozuiliwa kuondoka katika uwanja wa ndege wa Algeria walipowasili kwa mkumbo wa kwanza ,wakisema jezi hizo zilikuwa na ramani ya Morocco iliyojumuisha ramani ya taifa la Western Sahara.
USM Alger walikataa kufika uwanjani kwa mchuano huo baada ya ombi lao kwa CAF kutaka Barkane washurutushwe kubadilisha jezi, kutupiliwa mbali na wageni wakapewa ushindi wa ubwete.
Mchuano wa marudio Jumapili iliyopita pia haukuchezwa katika uwanja wa Manispaa wa Barkane nchini Morocco ilivyoratibiwa licha ya wageni USMA kuwasili Morocco na kulakiwa vyema Ijumaa.
Barkane pia walipewa ushindi wa bwerere wa magoli matatu kwa bila na kufuzu kwa fainali ya kombe hilo kwa ushindi wa jumla wa magoli 6-0 ,na watamenyana na Zamalek ya Misri katika fainali.
Algeria imekuwa ikiunga mkono kujitenga kwa taifa la Western Sahara huku Morocco ikisema Western Sahara ni sehemu yake, hali ambayo imechangia mzozo wa kidiplomasia tangu mwaka wa 2021.