Jeshi la Sudan limetwaa uwanja wa ndege wa Khartoum kutoka kwa RSF

Tom Mathinji and BBC
1 Min Read
Jeshi la Sudan limetwaa uwanja wa ndege wa Khartoum kutoka kwa wapiganaji wa RSF.

Jeshi la Sudan limesema limeuteka tena uwanja wa ndege katika mji mkuu, Khartoum, kutoka kwa wanamgambo wa RSF.

Kulingana na jeshi hilo, hatua hiyo inaashiria mafanikio yake ya hivi punde katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili.

Jenerali Mahomed Abdel Rahman al-Bilawi, amesema wanajeshi wameilinda kikamilifu na wanaweza kuwaondoa wapiganaji wengine wa RSF ifikapo mwisho wa siku.

Jeshi limekuwa likienda kwa kasi tangu kutwaa tena ikulu ya rais siku ya Ijumaa, na raia wamekuwa wakisherehekea barabarani linaposonga mbele.

RSF ilikuwa imedhibiti sehemu kubwa ya miji mikuu tangu vita vilipoanza Aprili 2023.

Nchini kote, mamia ya maelfu wameuawa, na mamilioni wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

Aidha msemaji wa jeshi alisemaa wanajeshi wameteka daraja la Manshiya, daraja la mwisho linaloshikiliwa na RSF, pamoja na kambi ya kijeshi katika ngome ya kusini mwa kundi hilo.Lakini vita bado havijaisha.

RSF bado inashikilia karibu eneo lote la Darfur magharibi mwa Sudan, ambapo mapema wiki hii, walioshuhudia walisema makumi ya raia waliuawa wakati jeshi la anga lilipolipua soko.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *