Jeshi la Israel lashambulia hospitali ya Al Shifa

Tom Mathinji
1 Min Read

Jeshi la Israel linasema limeshambulia hospitali kuu ya mji wa Gaza, Al Shifa,  katika operesheni inayolenga kambi kuu ya wapiganaji wa Hamas.

Kulingana na jeshi la ulinzi la Israel, kambi ya wapiganaji wa Hamas, iko chini ya jengo la hospitali lenya maelfu ya raia wagonjwa na waliopewa hifadhi huko.

Katika taarifa Jumatano alfajiri, jeshi hilo  lilisema shambulizi hilo lilitokana na  habari za kijasusi kwamba wanamgambo wa Hamas wana maeneo maalum katika hospitali hiyo

Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba kuna karibu wagonjwa 2,300, wafanyakazi na watu waliopoteza makazi ndani ya hospitali hiyo, ambao wamekwama kwa siku kadhaa kutokana na mapigano makali na mashambulizi ya mabomu kutoka angani.

Kabla ya shambulio hilo Rais Joe Biden wa Marekani, aliihimiza Israel kuchukua tahadhari kubwa kuhusiana na hospitali, akisema ni lazima kwa hospitali kulindwa.

Share This Article