Jeshi la Israel limekiri kukosea katika shambulizi lake lililofanywa katikati mwa Gaza juzi Jumapili.
Mamlaka za eneo la Gaza zimesema watu 12, wakiwemo watoto 8, waliuawa wakati wa shambulizi hilo lililotekelezwa katika kituo cha kusambaza maji.
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Israel, IDF amenukuliwa akisema mashambulizi ya anga yalimlenga mtu ambaye ni gaidi.
Kulingana naye, “kosa la kiufundi” lilisababisha silaha kuangukia “makumi ya mita kadhaa” kutoka eneo lengwa.
IDF imeelezea kusikitikia “madhara yoyote yaliyotokea kwa raia wasiohusika.”
Uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea.