Idara ya jeshi la Kenya limetanga zoezi la kuwasajili makurutu kati ya Agosti na Septemba mwaka huu katika kaunti zote 47.
Miongoni mwa nafasi zilizotangazwa ni General Service Officer (GSO) Cadets ,Specialist Officers, General Duty Recruits, Tradesmen/women, na Defence Forces Constables.
Kwenye tangazo la KDF wanaonuia kusajili sharti wawe kati ya umri wa miaka 18 na 26 kwa kazi za GSO Cadets na General Duty Rectuits na wasizidi umri wa miaka 30 kwa Specialist officers pamoja na Tradesmen and women.
Wanaume sharti wawe na kimo cha mita 1 nukta 6 na mita 1 nukta 52 kwa wanawake na uzani wa chini zaidi uwe kilo 54 nukta 55 kwa wanaume na kilo 50 kwa wanawake.
Wanaopania kuteuliwa wanapaswa kutuma maombi kupitia mtandao kufikia Agosti 20 huku wale watakaofaulu wakijuzwa kupitia magazeti ya humu nchini baina ya Septemba 17 na 24 mwaka huu