Jamii zinazoishi mpakani zatakiwa kutangamana kwa amani

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi ameelezea haja ya jamii zinazoishi mpakani kudumisha amani.

Akizungumza alipofungua rasmi kongamano kuhusu utangamano wa amani miongoni mwa jamii zinazoishi katika kaunti za Narok na Kajiado, Mudavadi alisema mipaka haipaswi kuwa kizingiti, ila inapaswa kuwa daraja la kufanikisha maendeleo.

Mudavadi alitaja ukosefu wa mipaka iliyobainishwa kuwa chanzo kikuu kinachodumaza maendeleo na utangamano wa kanda.

“Katika historia, maeneo ya mipakani yameghubikwa na umaskini, ukosefu wa usalama, mabadiliko ya tabia nchi, ukosefu wa chakula na maji miongoni mwa changamoto zingine,” alisema Mudavadi.

Aidha alisema hali ya kuwa waangalifu, itasaidia pakubwa katika utangamano wa amani miongoni mwa jamii za mpakani.

“Lengo letu ni kubadilisha maeneo ya mpakani kuwa chemichemi ya amani, kuimarisha biashara za mpakani na utangamano wa kanda.”

Kulingana na Mudavadi, maeneo ya mpakani yanapaswa kuchangia katika Pato la Kitaifa kupitia uwekezaji.

Kongamano hilo linalenga kupiga jeki ukuaji wa uchumi na utangamano wa amani katika maeneo ya mpakani.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *