Jamhuri ya Czech yatangaza maombolezo ya kitaifa kufuatia mauji ya watu 15

Dismas Otuke
1 Min Read

Jamhuri ya Czech imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku moja baada ya mwanafunzi wa umri wa miaka 24, kumuua babake kabla ya kuwaua watu wengine 14 na kuwajeruhi wengine 25 katika chuo kikuu cha Prague .

Shambulizi hilo la bunduki ndilo baya zaidi kuwahi kutokea katika Jamhuri ya Czech.

Rais Petr Pavel ametangaza Disemba 23, kuwa siku ya maombolezo ya kitaifa na kuagiza bendera ya taifa kupeperushwa nusu mlingoti na kimya cha dakika moja kabla ya hafla yoyote ya kitaifa.

Website |  + posts
Share This Article