Jamaa aliyevaa kijeshi ili kushawishi mwanamke ahukumiwa Tanzania

Rajabu alitaka kutumia sare hizo za kijeshi kutongoza mwanamke, akiamini kwamba zingeongeza uwezekano wake kumkubali.

Marion Bosire
1 Min Read

Jamaa mmoja nchini Tanzania kwa jina Rajabu Reli wa umri wa miaka 22 alijipata matatani baada ya kupatikana akiwa amevaa zare za jeshi ilhali yeye sio mwanajeshi.

Alikamatwa na maafisa wa usalama na kufikishwa atika mahakama ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza anakoishi, na alihukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani.

Hukumu hiyo ilitolewa Januari 7, 2025 katika shauri la jinai nambari 445 la mwaka 2025 na Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Evodius Kisoka

Katika kujitetea mbele ya mahakama, Rajabu alisema kwamba alivaa sare hizo ili kuongeza uwezekano wa binti aliyekuwa akimtongoza kumkubali.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 5 mwezi Disemba mwaka jana, katika Kijiji cha Kasisa, Wilaya ya Sengerema.

Rajabu aliiomba Mahakama hiyo imuachie huru kwa sababu alikuwa mkosaji wa mara ya kwanza, lakini ombi hilo likakataliwa na hakimu Kisoka.

Kisoka alimhukumu kifungo hicho ili iwe fundisho kwa Watu wengine wenye tabia kama ya Rajabu.

Kulingana na sehemu ya 99 ya sheria ya Ulinzi ya Tanzania ya mwaka 1966, ni hatia  kwa yeyote asiye na idhini rasmi kuvaa sare za jeshi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *