Bei ya mahindi kutangazwa wiki ijayo

Dismas Otuke
2 Min Read

Waziri wa Kilimo Mithika Linturi ameahidi kutangaza bei mpya ya serikali  kununua mahindi kutoka kwa wakulima wiki ijayo.

Maeneo mengi yanoyokuza mahindi nchini yanatazamiwa kuanza kuvuna kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.

Idadi ya mahindi yanayotazamiwa kuvunwa mwaka huu inatarajiwa kuongezeka kufuatia kuanzishwa kwa mpango wa serikali wa kutoa mbolea ya bei nafuu kwa wakulima.

Awali, Rais William Ruto alisema serikali idadi ya mahindi yanayotarajiwa kuvunwa mwaka huu kote nchini ni magunia milioni 61.

Hili litakuwa ongezeko la magunia milioni 17 ikilinganishwa na magunia milioni 44 yaliyovunwa mwaka jana.

“Mwaka uuliopita, tulivuna magunia milioni 44 kwa sababu wakulima hawakuweza kugharimia bei ya mbolea ambayo ilikuwa juu sana. Lakini mwaka huu, kwa sababu tumeweka mpango mzuri, tumepunguza gharama ya mbolea, mavuno ambayo tunatarajia ambayo yameanza kuja ni magunia milioni 61,” alisema Rais Ruto Agosti 17 wakati akitoa hotuba katika kanisa la ACK alikoweka jiwe la msingi la ujenzi wa kanisa hilo, kaunti ya Kiambu.

Rais William Ruto amehusisha mavuno mengi yanayotarajiwa na hatua iliyochukuliwa na serikali ya Kenya Kwanza mapema mwaka huu kupunguza bei ya mboolea kutoka shilingi elfu 7 hadi 3,500.

Halmashauri ya Nafaka na Mazao, NCPB itaanza kununua mahindi kutoka kwa wakulima kupitai kwa ghala zake zilizopo kote nchini, hususan maeneo ya North Rift.

Share This Article