Jamaa mmoja kwa jina Juma Msemwa amehukumiwa kifungo cha miaka 180 gerezani na mahakama moja ya wilaya ya Njombe nchini Tanzania kwa makosa ya ubakaji na ulawiti.
Msemwa mwenye umri wa miaka 27, alipatikana na hatia kwenye makosa sita ambayo yote yanahusiana na ubakaji na kila kosa likampa hukumu ya kifungo cha miaka 30 gerezani na atatumikia vifungo hivyo vyote kwa wakati mmoja.
Kando na kifungo hicho, Juma ametozwa faini ya shilingi milioni moja pesa za Tanzania kwa kila mwathiriwa.
Hakimu wa Njombe Matilda Kayombo, aliambia mahakama kwamba Juma alipatikana na makosa matatu ya ubakaji na matatu ya ulawiti kutokana na waathiriwa wake watatu.
Inaripotiwa kwamba aliwateka nyara na kuwabaka wanawake watatu kwa pamoja Mei 16 hadi 23 mwaka huu wa 2023 katika makazi yake mtaani Kihesa Kilimanji mjini Njombe.
Mmoja wa waathiriwa wake alifanikiwa kukwepa akipiga mayowe majirani walipokuja wakaokoa wenzake wawili kutoka kwa nyumba ya Juma naye akakamatwa.
Waathiriwa walielezea kwamba Msemwa alikuwa anawabaka kwa zamu kwenye sehemu zote na alipochoka alikuwa anaingiza vifaa kama gunzi kwenye sehemu zao za siri.
Alipohojiwa na mahakama, Juma alikiri makosa yake na kuelezea kwamba alikuwa anatekeleza maagizo ya mganga ambaye alimwelekeza abake wanawake na watoto.