Italia yanusurika Euro 2024

Martin Mwanje
2 Min Read

Mabingwa watetezi wa taji la bara Ulaya, ltalia walinusurika kulazwa na timu ya Croatia kwenye kipute cha Euro 2024 kinachoendelea nchini Ujerumani.

Katika mchuano huo uliosakatwa ugani Red Bull Leipzig, timu zote zilionyesha ujuzi mwingi huku zikikosa nafasi nyingi za wazi.

Mnamo dakika ya 55, Luka Modric alipachika bao baada ya kushindwa kufunga mkwaju wa adhabu.

Hata hivyo, Italia haikufa moyo kwani ilizidisha mashambulizi makali hadi dakika ya mwisho ya muda wa ziada (90+8) pale nguvu mpya Mattia Zaccagni wa klabu ya Lazio (Italia) alipovurumusha kombora zito wavuni.

Wakati huo huo, Uhispania walizoa alama zao zote tisa za kundi hilo la B illipoishinda Albania goli moja kwa bila kupitia winga wa klabu ya Barcelona Ferran Torres katika dakika ya 13.

Baada ya mechi hizo, Italia imejiunga na Uhispania kwenye awamu ya 16 bora na zitamenyana na washindi wa kundi D.

Croatia itasubiri hadi mwisho wa mechi za makundi kujua iwapo watapata nafasi katika timu nne za mwisho ila Albania imeaga mashindano hayo.

Leo Jumanne ni fursa ya kundi C na D. Ufaransa watakabana koo na Poland wakati Uholanzi wakimaliza udhia na Austria saa moja usiku. Itakapotimu saa nne usiku, Denmark watamenyana na Serbia nayo Uingereza ikamilishe dhidi ya Slovenia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *