Taarifa na BBC
Israel imethibitisha kuwa imetekeleza mashambulizi ya makombora nchini Iran Jumamosi asubuhi.
Akitangaza hayo, Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, alisema jeshi la Israel limewasha ving’ora vya tahadhari ya mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kuwaandaa wananchi kwa uwezekano wa kurushwa kwa makombora kuelekea Israel, kama hatua ya kulipiza kisasi.
Milipuko mitatu imesikika katikati mwa jiji la Tehran, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.
Shirika la Habari la Fars linasema kuwa limepokea taarifa kwamba makombora kadhaa yamepiga eneo mji mkuu wa Iran.
Kwa sasa Israel imefunga anga yake kwa safari za ndege za kiraia, kufuatia shambulio dhidi ya Iran Jumamosi asubuhi, kulingana na ripoti katika vyombo vya habari vya Israeli.